Friday, August 1, 2014

SALMA JABU NISHA AWA KIVUTIO CHA MASHABIKI WENGI KUTOKANA NA FILAM ZAKE KUFANYA VIZURI SOKONI

SALMA JABU NISHA

Salma Jabu Nisha  amekuwa kivutio cha mashabiki wengi na sasa ndio mmoja wa wasanii wakubwa hapa Tanzania anayeshika chati za juu katika filamu na hata mkwanja anaolipwasio wa kawaida na hii imetokana na filamu zake kufanya vizuri sokoni
FILAMU YA ZENA NA BETINA
 Akiongea na mkurugenzi wa blog ya hii bwana Thabit Shebe amesema tangu ameanza kufanya kazi zake mwenyewe chini ya kampuni yake ya NISHA'S FILM amekuwa akipokea pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki mbalimbali wa filamu nchini kwani filamu zake zimekuwa zikiangaliwa na watu wa rika zote kwasababu zimetengenezwa kwa kufata maadili ya Kitanzania.

 pia amesema amekuwa akipata mafanikio makubwa kutoka na filamu zake kufanya vzr sokoni hivyo kumuingizia mkwanja mnene..nisha kwa sasa anatamba na filamu inayoitwa ZENA NA BETINA ambayo ina wasanii wakali ndani yake kama vile HANIFA DAUDI (JENIFER), SENGA, HAPPY NYATAWE, MANAIKI SANGA na wengine kibao
Meneja wa blog hii bwana Thabit Shebe pamoja na wafanyakazi wake kwa ujumla wanamtakia kila la kheri katika kazi zake nzuri ambazo zimekuwa kivutio Tanzania na Afrika kwa ujumla.
SALMA AKIWA NA BEST CAMERA MAN KABUTI ONYANGO
                                            

No comments:

Post a Comment