Washtakiwa wakiwa katika gari la polisi
Washtakiwa wakisubiri kuingia mahakamani.
Wakipanda gari baada ya kusomewa mashitaka
Mkurugenzi wa
Mashitaka Nchini (DPP), aliwapandisha kizimbani vigogo wanne wa Chuo
Kikuu cha Kimataifa cha Tiba (IMTU) na baadaye kuwaondolea mashitaka
kupitia hati ya Nole ya kuwaondolea mashtaka ya kushindwa kufukia viungo
vya binadamu na kupeleka hati ya kufukia viungo vilivyotumika
kufundishia kwa Kampuni Coroner.
Vigogo hao
ni, Venkat Subbaian (57), Appm Shankar (64), Prabhakar Rao (59) na
Dinesh Kumar (27) ambao walisomewa mashtaka yao katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo saa 8:07 mchana.
Washtakiwa hao walisimama kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kwey
Lusemwa.
Mwendesha
Mashitaka wa Polisi, Magoma Magina alidai kuwa Julai 20, mwaka huu
washtakiwa wakiwa na nyadhifa tofauti, Profesa, Mtawala na wahadhiri,
kwa makusudi walishindwa kufukia mifuko 83 iliyokuwa na viungo vya
binadamu kinyume cha sheria ya 128 kifungu cha 8 na cha 9 cha Mwenendo
wa Makosa ya Jinai (CPA).
Magina alidai
kuwa katika shitaka la pili, washtakiwa wote kwa pamoja walishindwa
kupeleka hati ya kumtarifu kwamba wamefukia viungo hivyo baada ya
kutumika kufundishia kama sheria inavyowataka.
Hakimu Lusemwa alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania kila mmoja.
Hakimu Lusemwa alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania kila mmoja.
Hata hivyo,
kabla mahakama haijasikiliza kipengele cha dhamana, Wakili wa Serikali
Mwandamizi, Salum Ahmed aliwasilisha hati ya Nole kutoka kwa DPP akidai
kuwa anawaondolea vigogo hao mashtaka na kwamba hana nia ya kuendelea
kuwashitaki.
Ahmed alidai
kuwa DPP anawaondolea washtakiwa mashitaka hayo chini ya kifungu cha 91
kidogo cha (1) cha CPA kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaka.
Wakili wa washtakiwa Gaudiosus Ishengoma alisema kwamba inaonekana kuna mbinu kubwa dhidi ya washtakiwa.Alisema
anavyofahamu kwamba hati ya mashitaka ingekuwa na kasoro wateja wake
wangepata dhamana na baadaye ingewezekana kubadilishwa.
Alisema
kutokana na sababu hiyo, ana wasiwasi kwamba inawezekana DPP ana nia ya
kuwafungulia wateja wangu kesi yenye mashitaka yasiyokuwa na dhamana ili
wakasote mahabusu.
Viwanja vya
mahakama hiyo vilikuwa tulivu huku wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa IMTU
wakiwa wamesimama katika makundi makundi wakijadiliana hili na lile.
Kupitia
magari ya Jeshi la Polisi, T 366 AVG aina ya Rav4 alipanda mshtakiwa wa
tatu kwa madai kuwa ni mgonjwa na washtakiwa wengine waliondoka
mahakamani hapo katika gari yenye namba za usajili KX06EFY aina ya
Toyota Landcruiser na kurudishwa mahabusu ya jeshi hilo.




No comments:
Post a Comment