Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekie l(kulia) akiwa na shosti yake Wema sepetu.
Aunt alifunguka hayo mara baada ya kuulizwa na mwanahabari wetu juu
ya mtazamo wake kuhusu mapenzi ya wawili hao ambapo alisema mapenzi yao
yamekuwa yakimvutia na kila mmoja anaonekana kuwa na mapenzi ya kweli
kwa mwenzake hivyo hawezi kupendezwa hata siku moja akiona hawapo
pamoja.
Wema sepetu na mpenzi wake Daimond Platinum wakiwa ni wenye furaha.
“Kusema kweli naona hawa watu wanapendana na kujaliana sana, siku
zote nawaombea kwa Mungu mapenzi yao yadumu milele na ninaamini
watafikia malengo yao, sitapenda hata siku moja kuona wapo tofauti,”
alisema Aunt.


No comments:
Post a Comment