Kova akionyesha baadhi ya sare za jeshi la polisi alizokamatwa nazo polisi huyo feki.
JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam linamshikilia
na kumhoji mtu mmoja anayeitwa Robson Seif Mwakyusa (30) mkazi wa
Kijitonyama Jijini Dar, kwa tuhuma za kujifanya ofisa wa polisi kikosi
cha usalama barabarani huku akifanya ukaguzi wa makosa ya usalama
barabaraniMtuhumiwa huyu alikamatwa umamosi iliyopita huko Kata ya Chamazi, Mbagala-Majimatitu Mkoa wa Kipolisi Temeke akiwa amevalia sare za polisi na cheo cha stesheni sajenti na akiwa na leseni mbalinbali za magari, ‘radio-call’, stakabadhi, na vitu vingine.
No comments:
Post a Comment