Tuesday, August 5, 2014

SHABIKI MKUBWA YA YANGA WAKULIALIA AIKIMBIA YANGA!!

                              
Dar es Salaam. Unakumbuka yule shabiki wa Yanga maarufu kwa jina la Steve Yanga au Shabiki wa kulialia?, SasaNni kwamba ameibuka na kihoja kipya baada ya kutangaza kutoishabikia tena timu hiyo na kusema yuko njiani kuhamia Simba au Azam FC.
Akizungumza na gazeti hili jana, Steve ambaye aliwahi kuzawadiwa pikipiki na mMwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji kutokana na kuwa na mahaba mazito na klabu hiyo, alisema ameamua kuikacha timu hiyo baada ya kukwaruzana na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo.
                              
“Ukweli ni kwamba, Yanga imenifanya niwe mtu maarufu ndani na nje ya nchi, lakini nimeamua kuacha kuishabikia tena baada ya kutukanana na viongozi.
“Kuna siku nilimpigia simu na kiongozi mmoja wa zamani wa Yanga wa zamani (jina tunalihifadhianamtaja), alinitukana kisha akakata simu. H, hili tukio lilinikwaza sana ndiyo maana nimechukua uamuzi huo,” alisema Steve.
”Kwa sasa natafakari kwanza, lakini nipo njiani kuhamia timu moja wapo kati ya Simba au Azam FC.,”.
Wakati Steve akichukua uamuzi huo, shabiki mwingine maarufu wa klabu hiyo Ali Mohamed ‘Ali Tumbo’ alisema kitendo kilichofanywa mwenzake ni kujidhalilisha.
“Hata mimi napenda fedha, lakini siyo kwa staili iliyofanywa na huyu Steve. H, huku ni kuendekeza njaa kulikopitiliza... ,yaanin amejidhalilisha,,” alisema.

No comments:

Post a Comment