KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kwamba hawezi kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake,
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’,
Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati, Diamond alitoa kauli hiyo
na kuandikwa kwenye ukurasa wa mbele wa blog hii likiwa na kichwa cha habari; ‘DIAMOND HAFIKIRII KUOA ambapo ndani yake alieleza jinsi ambavyo mastaa wengi waliooa
wameanguka kisanii.
MTU WA KARIBU AYASEMA YA WEMA
Kwa mujibu wa mtu
wa karibu wa mastaa hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo kwa sababu
anajua yeye ndiye mke mtarajiwa wa Diamond.
Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza ile furaha ya kwamba wawili
hao wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama ilivyotabiriwa na mnajimu
maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya Hussein.
“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na kutotimia kwa utabiri wa Maalim
Hassan kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi ya tukio hilo muhimu
kwenye maisha ya mwanadamu, Wema ameanza kukata tamaa, lakini amesema
hawezi kulazimisha ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si utamaduni wa wanawake
wa Kitanzania wala Kiafrika.
“Unajua Kibongobongo au hata Kiafrika hai-sound vizuri na pengine
haiwezekani kwa mwanamke kulazimisha kuolewa kama mwanaume hataki. Hicho
ndicho kilichomtibua Madam (Wema) baada ya kusoma alichokisema
Diamond,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Wema amehisi yeye ni girl lover (mpenzi) tu kwa Diamond na si wife
material (mke mwema) kwa hiyo anawaza sana kuhusiana na ishu hiyo japo
mahaba niue kati yao yanaendelea, lakini anafikiria kuchukua uamuzi
mzito.”
WEMA SASA
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti
hili lilimtafuta mlimbwende huyo anayeshikilia Krauni ya Miss Tanzania
2006 ili kumsikia mwenyewe ambapo alifunguka yake ya moyoni.
Mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa haumizi tena kichwa kuhusu suala la ndoa na Diamond na kwamba hana haraka nalo.
“Mimi naamini sana mambo ya utabiri, lakini siumizi kichwa na suala la kuolewa na Diamond na kamwe siwezi kumlazimisha anioe.
“Kikubwa katika mapenzi ni upendo wa kweli ambao ananionesha bila
kipimo. Wala sina papara, hata kama mtabiri kasema ndoa yetu ni lazima
ifungwe mwaka unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya mwaka 2016 kama
itashindikana mwezi huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie
kuolewa na Chibu (Diamond).
“Ninachojua mimi Mungu ndiye anapanga yote na kama ndoa ipo ipo tu
maana kuna watu wapo kwenye ndoa na hawana upendo wa kweli kama
tulionano sisi,” alisema Wema.
MAMA WEMA ANASEMAJE?
Paparazi wetu alimtwangia
simu mama yake Wema, Mariam Sepetu na kumuuliza mambo mawili, kuhusu
bintiye kuvishwa pete ya ndoa na Diamond na suala la Mbongo Fleva huyo
kusema hataoa kamwe!
“Mimi niseme nini? Sina la kusema kuhusu Wema.
Mambo yake ni yake mwenyewe na huyo Diamond wake. Kwanza kwa nini
mnipigie mimi, si mumtafute yeye mwenyewe?” alisema mama huyo kwa sauti
ya utulivu.
MAMA DIAMOND AFUATA NYAYO
Katika hali ya
kushangaza, mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ ameonekana kunawa mikono
kwa kauli aliyowahi kuitoa siku za nyuma kuhusu mtoto wake na masuala
ya kutooa au kuoa.
Nasibu ni mtu mzima sasa, siwezi kumpangia lolote kuhusu kuoa au
kutooa. Wakati ukifika, anaweza kusema lolote ambalo ataliona ni zuri
katika maisha yake.”
KUHUSU PETE YA NDOA
Kuhusu Diamond kumvisha pete
ya ndoa Wema, tendo ambalo lilifanyika hivi karibuni wakiwa nchini
Afrika Kusini, Amani lilifanikiwa kuzungumza na shehe mmoja ambaye
aliomba hifadhi ya jina lake ambapo alisema alichokifanya Diamond kwa
Wema ni usanii.
“Diamond amemfanyia usanii mwenzake. Pete gani bila kufunga ndoa.
Halafu katika Uislam, hakuna tendo la wanandoa kuvalishana pete, hayo
mambo wanayafanya wenyewe, ” alisema shehe huyo.
WEMA AIZUNGUMZIA PETE
Wema alipopewa nafasi ya
kuizungumzia pete hiyo alisema Diamond aliipenda tu akaamua kumnunulia
na kumvisha lakini haihusiani na ndoa.
“Sisi (na Diamond) tulikuwa Afrika Kusini, baby wangu akaipenda pete,
akainunua na kunivalisha, haina uhusiano na ndoa,” alisema Wema




No comments:
Post a Comment