BREAKING NEWS!! BASI LA MORO BEST LAPATA AJALI, LAUA WATU 20
Basi la Moro Best baada ya ajali hiyo mbaya.
Majeruhi
wakiwa wamelala na kukaa baada ya basi la Moro Best lililokuwa linatoka
Mpwapwa kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori eneo la
Pandambili.
Muonekano wa Basi la Moro Best baada ya ajali.
Baadhi ya majeruhi wa ajali wakipelekwa Hospitali ya Mkoa Dodoma huku wengine wakipelekwa Hospitali ya Mpwapwa.
TAKRIBANI watu 20 wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wengi
wakijeruhiwa baada ya basi la Moro Best lililokuwa linatoka Mpwapwa
kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori eneo la Pandambili,
Kongwa mkoani Dodoma leo. Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa
katika Hospitali ya Mkoa Dodoma huku wengine wakipelekwa Hospitali ya
Mpwapwa.
No comments:
Post a Comment