Jamani! Katika hali ya kushangaza, mastaa wa filamu Bongo wamesusia kumbukumbu ya siku 40 ya aliyekuwa muongozaji maarufu wa filamu nchini, George Otieno ‘Tyson’ aliyefariki dunia kwa ajali Mei 31, mwaka huu.
Aliyekuwa mke wa George Otieno, 'Tyson', Beatrice Shayo
Shughuli ya 40 ya Tyson ilifanyika Alhamisi iliyopita nyumbani kwa
aliyekuwa mkewe, Beatrice Shayo maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo
mastaa mbalimbali walialikwa lakini hakuonekana hata mmoja hali
iliyosababisha chakula na futari iliyokuwa imeandaliwa kubaki huku
wasanii wa vikundi waliohudhuria wakirudia mara mbilimbili.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba
Akizungumza na gazeti hili, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
(TAFF), Simon Mwakifwamba aliyekuwa kwenye shughuli hiyo alisema
anashangaa mastaa wa filamu kukacha ishu hiyo kwani alimpa taarifa
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kwamba
awaambie wahudhurie.“Nimewaalika wasanii wote lakini hakuna aliyekuja hata mmoja, ukweli wasanii hatuna ushirikiano kwani Tyson ndiye mwanamapinduzi aliyeigeuza sanaa kutoka kwenye kuuza sura hadi kuwa biashara hivyo walipaswa kumpa heshima yake,” alisema Mwakifwamba.

No comments:
Post a Comment