Memba wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhan ’Tunda Man’
amekutwa na mauzauza baada ya kupokea simu yenye namba zinazodaiwa kuwa
za ajabu na kumsababishia atokwe damu puani, mdomoni na kupooza upande
mmoja.
Thursday, July 31, 2014
Wednesday, July 30, 2014
UINGEREZA KUANZA KUTUMIA MAGARI BILA DEREVA MWAKANI
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa itaziruhusu gari zisizokuwa na madereva barabarani ifikapo mwezi Januari mwakani.
UNDANI WA BIFU LA RAY NA CHIKI
BAADA ya kuibuka sintofahamu kati ya waigizaji wa
Bongo Movies, Salum Mchoma ‘Chiki’ na Vincent Kigosi ‘Ray’, Chiki
ameibuka na kuzungumzia ishu hiyo.
NDOA YA LUCY KOMBA MIZENGWE, CHANZO CHETI CHA UKIMWI
HUKU akiwa kwenye vikao vya maandalizi ya harusi na
Mzungu, staa wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba (pichani na mchumba
wake), amejikuta katika wakati mgumu baada ya habari kudai kwamba,
mchumba wake huyo amemwambia ili ndoa ifungwe lazima aoneshe cheti cha
kipimo cha Ukimwi kwanza.
PICHA; DIAMOND PLATNUMZ APELEKA TUZO TANDALE!
Mwamuziki wa Kizazi Kipya,Naseeb Abdul (Diamond Platnumz ) akiwa amezungukwa na Mashabiki ambao wakati alipota katika barabara ya kwa mtogole kupeleka tuzo yake kwa mama yake ambaye anaishi Tandale kwa Mtogole jijini Dar es Salaam jana akitokea nchi Marekani alikopata Tuzo ya AFRIMMA 2014.Picha na Humphrey Shao.
MAPYA YAIBUKA KUHUSU SAKATA LA KUTUPWA VIUNGO VYA BINADAMU
SAKATA la kutupwa kwa viungo vya binadamu
lililofanywa na Chuo Kikuu cha Tiba cha Kimataifa cha IMTU kilichopo
Mbezi jijini Dar, linadaiwa kuikumba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
baada ya tanuru linalotumika kuteketeza viungo vya binadamu kuharibika
kwa miezi sita sasa.
SANGOMA AKATA NYETI ZA MTOTO MDOGO
NI jambo lililowaacha midomo wazi madaktari na wauguzi wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam ambapo mtoto Almasi
mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi (pichani akiwa na muuguzi)
kufikishwa hospitalini hapo akiwa amekatwa nyeti na mtu aliyedaiwa ni
mganga wa kienyeji ‘sangoma’ na kuipeleka kusikojulikana.
MTANZANIA ANAYESAKWA KWA KESI YA MAUAJI AONESHA JEURI YA FEDHA
WAKATI akisakwa kwa udi na uvumba na serikali ya
Tanzania ili kuunganishwa katika kesi ya mauaji jijini Dar es Salaam,
mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe anadaiwa kufanya jeuri ye
fedha nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’.
Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe akiwa ndani ya gari.
MR.NICE NA SIRI YA KUFILISIKA KWAKE,ATOA NENO KWA DIAMOND
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Lucas Mkenda ‘Mr
Nice’ ameibuka na kufunguka kuwa siri ya kufilisika kwake ni kupenda
kwake sifa kutoka kwa wapambe na matumizi mabaya ya fedha alizokuwa
akiziingiza.
GARI LA MSANII DUDE LAKAMATWA KWA UJAMBAZI
GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.
MSANII MWINGINE WA BONGO AKAMATWA CHINA!

HUKU modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na polisi nchini humo.
Monday, July 28, 2014
MAJINA YA WALE WALIOCHAGULIWA NAFASI ZA KAZI UHAMIAJI NA MAJINA YA NDUGU ZAO!!
Matokeo
ya Usaili wa nafasi za kazi Uhamiaji yaliyotolewa katika magazeti
mbalimbali mwezi Julai, 2014 yameonesha kuwa katika dara hiyo watanzania
wengine mbali ya watoto au ndugu wa wafanyakazi wa idara hiyo hawawezi
kupata ajira ndani ya idara hiyo ya Serikali kirahisi na hiyo inatokana
na ukweli kwamba majina ya wengi walioitwa kazini ni watoto au ndugu wa
wafanyakazi wa idara hiyo kama jinsi majina yanavyoonekana hapa chini:
MKE WA MSANII WA VICHEKESHO KINGWENDU ABAKWA!!

MKE wa Kingwendu ambaye ni muigizaji maarufu wa filamu za vichekesho nchini amefanyiwa kitendo kibaya cha ubakaji na mwanaume aliyefahamika kama Upunguvuku katika pagala moja huko Mbagala Kingugi kwa Kisauti.
CHEKI HII; MAAJABU YA MCHEZO WA SOKA WA KENGELE KWA VIPOFU

“Kabla ya kuanza mechi, kocha unatakiwa kumchukua mchezaji mmoja mmoja na kumzungusha eneo zima la uwanja kwa dakika 30, tunafanya hivyo ili kumjengea mchezaji hali ya kuzoea mazingira ya uwanja kabla ya kucheza,” anasema kocha wa mpira wa kengele, Hashiru Tembo
Sunday, July 27, 2014
MASTAA WASUSIA 40 YA MAREHEMU GEORGE TYSON
BAHATI BUKUKU APATA AJALI NA KUUMIA VIBAYA
NI kweli ajali haina kinga! Nyota wa nyimbo za
Injili Bongo, Bahati Lusako Bukuku ameumia mgongo na maeneo kadhaa ya
mwili (nusu kifo) kiasi cha kushindwa kukaa, kusimama wala kutembea
kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea kwenye eneo la Ranchi ya Narco
wilayani Kongwa, Dodoma saa tisa usiku wa kuamkia Jumamosi, Ijumaa
Wikienda lina undani wa mkasa mzima.
SAKATA LA KUOKOTWA VIUNGO VYA BINADAM; MUHAS YASEMA: Tunatumia maiti 25 kwa mwaka kufundishia

Wakati sakata la kuokotwa kwa viungo vya binadamu likiendelea kutikisa nchi, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kimesema kuwa hutumia maiti 25 kwa kuwafundishia wanafunzi kila mwaka.
Saturday, July 26, 2014
BIFU LA ALI KIBA NA DIAMOND LAFIKIA PABAYA! ALIKIBA AELEZEA KISA CHA UGOMVI
Hatimaye! Kwa mara ya kwanza staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na
nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba ameibuka na kumlipua hasimu wake, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, hali inayotafsiriwa kwamba bifu lao sasa
limefika pabaya ikidaiwa kwamba wanagombea nyota (ustaa).Friday, July 25, 2014
"YESU KRISTO HATORUDI TENA"-MSEMAJI WA VATICAN KANISA KATOLIKI ATANGAZA RASMI
Msemaji wa Vatican (Roman Catholic) ametangaza rasmi leo kwamba ujio wa
pili wa Yesu, mtoto wa pekee wa Mungu, unaweza usitokee tena, lakini
amewahimiza wafuasi wa kanisa Katoliki kuendelea na imani yao, bila
kujali taarifa hiyo.
Thursday, July 24, 2014
TIMBWILI GESTI! MJOMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPWA WAKE
TIMBWILI la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani.

MABAKI YA NDEGE YA ALGERIA YAONEKANA
Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali.MAZITO 10 YAIBUKA: VIUNGO VYA BINADAMU KUNASWA DAR!
Lile sekeseke la viungo vya binadamu kukutwa kwenye dampo jijini Dar es Salaam limechukua sura mpya huku mambo mazito 10 yakiibuliwa.
Subscribe to:
Comments (Atom)















