Friday, August 15, 2014

BABA AMBAKA MWANAYE WA KUMZAA AKITAFUTA UTAJIRI



Sumbawanga. Polisi wilayani hapa inamshikilia mkazi wa Kijiji cha Lwanji, Bonde la Ziwa Rukwa, Edwin Kachele (30) kwa tuhuma ya kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 11 kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

MUME WA MTU NAYE NI SUMU, ONA MWANAMKE ALIVYOHARIBIWA USO NA MAFUTA YA MOTO!

Mbuva, akiwa na majeraha usoni baada ya kumwagiwa mafuta ya moto.
Mbuva, akiwa na majeraha usoni baada ya kumwagiwa mafuta ya moto.
MWANADADA aliyefahamika kwa jina moja la Mbuva, mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar, hivi karibuni amejikuta akiharibiwa uso wake kwa kumwagiwa mafuta ya moto na shosti wake aitwaye Mama Sofia, kisa kikidaiwa ni mume wa mtu.

WEMA AJIBU MAPIGO YA DIAMOND, ASEMA HAMPENDI HALIMA KIMWANA

     


Wema Sepetu a.k.a Beautiful Onyinye amekula kiapo cha kumchukia dada wa hiyari wa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’, Halima Kimwana ambaye wamekuwa na bifu kwa kipindi kirefu huku sababu zikiwa hazijulikani.

Thursday, August 14, 2014

PENZI LA WEMA & DIAMOND LAFIKIA MWISHONI, DIAMOND AMPA DONGO WEMA


STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amemtupia vijembe mpenzi wake Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram usiku huu akionekana kuchukizwa na tabia ya staa huyo kupenda maisha ya starehe zisizo na faida.

ASKOFU WA ARUSHA ATUPWA JELA MIAKA 32 KWA UJAMBAZI!

                                      


Askofu wa Kanisa la Christian Fellowship Assemblies of God la Arusha, Jumanne Kilongola amehukumiwa kifungo cha miaka 32 jela baada ya kupatikana na hatia ya kupora Sh5.3 bilioni ndani ya Benki ya NBC, Tawi la Moshi Mei 21, 2004.

HATIMAYE JACK PATRICK AHUKUMIWA KWENDA JELA BADALA YA KUNYONGWA

BAADA ya kushikiliwa kwa takriban miezi tisa kwa kesi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye Video Queen maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu ikawa ndogo zaidi, Amani linaibumburua habari kamili.
 

Wednesday, August 13, 2014

MZEE WA MICHEPUKO KIBONDE, GADNA HABASH WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gadna Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kutoa lugha ya matusi.

AUNT EZEKIEL ANASWA LAIVU NA MUME WA MTU!

STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa na vituko, Aunt Ezekiel amenaswa live akijivinjari na mume wa mtu, Risasi Mchanganyiko linaripoti bila woga.
 

MZUNGU AINGILIA PENZI LA WEMA, ANATAKA KUISHI NAYE ULAYA!

MALOVEE? Mzungu aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’ anadaiwa kuingilia penzi la mwigizaji Wema Sepetu.
Ishu hiyo imebumburuka ikiwa ni siku chache tangu Diamond atangaze kuwa hayupo tayari kuoa akidai atashuka kimuziki.
 

Monday, August 11, 2014

MAHABA NIUE; DIAMOND NA JOKATE WAONEANA AIBU BAADA KUKUTANA LAIVU

Kwa mara ya kwanza tangu walipomwagana, mastaa wawili Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wanadaiwa kuoneana aibu walipokutana laivu.
 
Mastaa wawili Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ pichani.

KUMBE NEY WA MITEGO NDO SABABU YA DIAMOND KUSEMA HAYUPO TAYARI KUOA!

IMEVUJA kwamba Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ndiye aliyemshauri Nasibu Abdul ‘Diamond’ asioe kwa sasa ili asishuke kimuziki.

NJEMBA YA MIAKA 30 AMBAKA MTOTO WA MWAKA 1 KWA SAA 9!

USIPOSTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni, ni kweli kabisa! Mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja tunayemtaja kwa jina moja la Devota wa Sokoni One jijini hapa, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kufuatia kubakwa na njemba moja iitwayo Rajabu Mkoba (30), mkazi wa eneo hilo.
 

Sunday, August 10, 2014

JACK PATRICK AYEYUKA GEREZANI CHINA! HAJULIKANI ALIPO!

Video Queen wa Bongo anayeshikiliwa na jeshi la polisi nchini China kwa msala wa madai ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ anadaiwa kuyeyuka gerezani.

Saturday, August 9, 2014

WAKATI WASANII WAKIACHA BASHARA YA ALBUM, TID ALETA ALBUM YA 7

                       
Wakati idadi kubwa ya wasanii wa Bongo Fleva nchini wakikacha biashara ya kurekodi albamu na kutafuta njia mbadala ya kuuza muziki wao, mwanamuziki wa siku nyingi Khalid Mohamed maarufu (TID, Top In Dar), amesema anatarajia kutoa albamu yake ya saba.

VIDEO NA PICHA; MZEE WA MICHEPUKO SIO DILI EPHRAIM KIBONDE AKAMATWA NA POLISI!!

Akitaitiwa na trafikiMtangazaji maarufu wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Ephrain Kibonde leo ameshuhudia jinsi ambavyo mkono wa sheria ulivyo mrefu hata kwa mtu maarufu kama yeye alipojikuta kwenye wakati mgumu baada ya kusababisha ajali na kujaribu kukimbia. CHEKI VIDEO YAKE HAPA

BIASHARA CHAFU: Mwanafunzi chuo kikuu alazimishwa kurekodi picha za ngono

Sunday Bekunda
                                 
Kweli dunia ina mambo! Kuna watu wanajaribu kutumia kila fursa inayopatikana kujinufaisha kwa kupata fedha hata ziwe ‘chafu’, kwao kitu cha maana ni kupata utajiri kwanza.
Kundi la watu wanaofanya biashara ya kusafirisha watu, wamekuwa wakitumia fursa ya ukosefu wa ajira kama chambo cha kuwanasa vijana na kuwaingiza kwenye biashara haramu kama ukahaba.

Thursday, August 7, 2014

AGNES MASOGANGE AZUIWA UWANJA WA NDEGE, AHOJIWA KWA MASAA 9!

Dar es Salaam. Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kimemhoji kwa zaidi ya saa 10, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kuhusiana na tuhuma za kukamatwa na dawa aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini, Julai mwaka jana.

MAMA MJAMZITO WA MIEZI 9 AOGELEA MTONI KUTAFUTA HOSPITALI

Mwanamke mmoja nchini India ameogelea kwenye mto uliokuwa umejaa maji mengi yaliyotokana na mvua kubwa ilhali akiwa na ujauzito wa miezi tisa.
                   

NEY WA MTEGO ASEMA ALIKUWA MWIZI BALAA!

CONFESSION! Kwa mara ya kwanza staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kuuelezea upande wa pili wa maisha yake kuwa kabla hajawa mwanamuziki alikuwa mwizi balaa!
Akizungumza na paparazi wetu ana kwa ana jijini Dar es Salaam juzi, staa huyo alikiri kupitia katika majanga kibao maishani mwake likiwemo la kulala katika vituo mbalimbali vya polisi vya jijini Dar kufuatia kufanya matukio ya uhalifu.
 

BAADA YA KUBWAGANA KWA SIKU CHACHE NUH MZIWANDA NA SHILOLE WARUDIANA

Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake Shilole.
 

PENZI LA WEMA NA DIAMOND KUVUNJIKA? WEMA AZUNGUMZA YA MOYONI

KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba hawezi kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua mwandani wake, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’,
 
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi.

Tuesday, August 5, 2014

SHABIKI MKUBWA YA YANGA WAKULIALIA AIKIMBIA YANGA!!

                              
Dar es Salaam. Unakumbuka yule shabiki wa Yanga maarufu kwa jina la Steve Yanga au Shabiki wa kulialia?, SasaNni kwamba ameibuka na kihoja kipya baada ya kutangaza kutoishabikia tena timu hiyo na kusema yuko njiani kuhamia Simba au Azam FC.

MLEMAVU AKAMATWA AKIUZA MADAWA YA KULEVYA DAR

                                 
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, limemkamata mkazi wa Vijibweni, Said Tindwa kwa kosa la kufanya biashara ya dawa za kulevya aina ya cocaine na heroine.

Monday, August 4, 2014

POLISI FEKI ALIYEKAMATWA AKUTANA NA KOVA!

 

MBOTO AWEKA WAZI KUHUSU TAARIFA YA BIFU LAKE NA WEMA

BIFU? Komediani Haji Salum ‘Mboto’ amekanusha vikali kuwa na bifu na Wema Sepetu baada ya tetesi za chinichini kuvuma kwamba wapo kwenye bifu zito.

AUNT ALIANGUSHIA MAOMBI PENZI LA DIAMOND, WEMA

KUTOKA moyoni? Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa siku zote amekuwa akimuombea dua shosti wake, Wema Sepetu ‘Madam’ na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ uhusiano wao udumu.
 

ALI KIBA ATAMKA WAZI KUWA LULU NI WIFE MATERIAL, AMMWAGIA SIFA KIBAO!

HII ni exclusive! Kwa mara ya kwanza, staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka kuwa mwigizaji kiwango Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa kuwa mke (wife material) huku akiweka wazi sifa kibao alizonazo, Wikienda liko bize kukujuza.

Friday, August 1, 2014

DIAMOND NAE AWAPONDA WAONGOZAJI WA FILAMU TANZANIA!

                                               


Pamoja na kutafuta video zenye kiwango cha juu zaidi, dharau na mapozi ni sababu kubwa zilizomfanya Diamond aache kushoot video zake kwa kutumia waongozaji wa video nchini.

SALMA JABU NISHA AWA KIVUTIO CHA MASHABIKI WENGI KUTOKANA NA FILAM ZAKE KUFANYA VIZURI SOKONI

SALMA JABU NISHA

HIKI NDICHO ALICHOAMUA KINGWENDU BAADA YA MKE WAKE KUBAKWA!

 

DIAMOND PLATNUMZ ASEMA HAFIKIRII KUOA KWA SASA! AHOFIA KUSHUKA KISANII


Kutoka moyoni? Wakati bimkubwa Wema Isaac Sepetu akijiaminisha na kuhisi kuwa amepata mume ambaye ni baba bora, mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kuwa kamwe hafikirii kuoa, Ijumaa lina cha kukuhabarisha.